Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja na mimi.@Ufunuo wa Yohana 3:20
picha
Rufus H. McDaniel
1850–1940

Rufus H. McDaniel, 1914 (Since Jesus Came into My Heart); . McDaniel aliandika haya maneno kama mwana wake, kijana, alikufa.

Charles H. Ga­bri­el, 1914 (🔊 pdf nwc).

picha
Charles Gabriel (1856–1932)

Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.

Refrain

Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu.

Refrain

Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu.

Refrain

Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu.

Refrain

Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu.

Refrain